Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Maliasili na Utalii kumuenzi Mwalimu Nyerere Butiama

Nyereeepic Data Christowaja Ntandu

Mon, 28 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake imeandaa mambo mbalimbali katika kuadhimisha miaka 100 ya baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika wilayani Butiama, ambapo kabla ya kilele kitakachofanyika Aprili 13, kutakuwa na midahalo itakayoendeshwa na taasisi za elimu ya juu nchini kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere na machango wake katika ustawi wa taifa.

Akizumgumza na waandishi wa habati mjini hapa baada ya kikao cha maandalizi ya maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Malikale kutoka wizara hiyo, Dk Christowaja Ntandu amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kumuenzi hayati baba wa taifa ambaye angekuwa hai angetimiza miaka 100 Aprili 13 mwaka huu.

"Mbali na maonyesho ya kila taasisi kutoka wizarani yatakayofanyika hapa Butiama lakini pia kuna taasisi kama ile ya Mwalimu Nyerere watafanya mdahalo tarehe 25 vyuo vingine pia vimethibitisha kuandaa midahalao kama hiy," amesema.

Ametaja vyuo ambavyo tayari vimethibitisha kuandaa midahalo kuwa ni pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam na kile cha Kumbulumbu ya Mwalimu Nyerere cha Kigamboni huku vingine vikiwa bado kwenye maandalizi.

Dk Ntandu amefafanua kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  wamekubaliana kuadhimisha miaka 100 ya mwalimu kwa kufanya shughuli mbalimbali kwa mwaka mzima ili kutoa nafasi kwa jamii kushiriki katika kumenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Advertisement

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Butiama, Moses Kaegele amesema kuwa wilaya yake iko tayari kwa ajili ya maadhimisho hayo kwani yanalenga kuendelea kuchocheo jamii na serikali kuendelea kumuenzi baba wa Taifa kwa vitendo.

"Baba wa Taifa alilitaka taifa kupambana na maadui ambao ni umasikini, maradhi na ujinga, hadi sasa serikali imekuwa kinara katika kupigana vita hivyo kwani tunaona namna ambavyo sekta za elimu, afya na uchumi zinavyoboreshwa kwa hiyo maadhimisho haya yataongeza chachu kwa jamii na wadau kuendelea kupambana," amesema Kaegele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live