Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Kilimo yatangaza punguzo la bei ya mbolea ya kupandia

73315 Kilimopic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga ametangaza punguzo la bei ya mbolea ya kupandia (DAP) akiwataka wakulima wachangamkie mbolea hiyo kwa msimu wa kilimo 2019/20.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 28, 2019 jijini Dar es Salaam, Hasunga amesema kutokana na ushindani wa zabuni kupitia mfumo wa ununuzi wa mbolea wa pamoja (BPS), bei za DAP zimeshuka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na zabuni ya Julai 2018.

"Ushindani wa zabuni za BPS pamoja na marejeo ya kikokotoo umefanya bei ya mbolea kwa mkulima kupungua kwa wastani kimkoa Sh8,000 hadi Sh10,000 sasa na asilimia 13 hadi 17 kwa mfuko wa kilo 50 wa mbolea aina ya DAP," amesema Waziri Hasunga.

Amesema kwa mfuko wa kilo 25 umekuwa na punguzo la kati ya Sh5,000 na Sh6,000 sasa na asilimia 14 hadi 19.

"Kwa muktadha huo, bei ya mbolea ya DAP kwa mikoa ya Kanda ya Mashariki, Kati, Kusini na Kati na Kaskazini zitakuwa kati ya Sh51,900 na Sh60,000.”

"Mikoa ya Kanda ya Magharibi Nyanda za Juu Kusini na Ziwa, bei elekezi itakuwa kati ya Sh57,000 na Sh63,200," amesema Hasunga akiongeza kuwa bei hizo zitaanza kutumika Septemba 1, 2019.

Pia Soma

Amesema mahitaji ya mbolea kwa msimu ujao yatakuwa tani 614,000 ambapo tani zaidi ya 150,000 za DAP zitahitajika huku akisema mpaka sasa kuna tani 56,310 za mbolea hiyo zilizobaki mwaka 2018.

"Kwa jumla mbolea iliyopo mpaka leo ni tani 205,435 tunayo kama bakaa iliyopo," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz