Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Kilimo yaanda marekebisho madogo ya sheria

Kilimo Marekebisho Wizara ya Kilimo yaanda marekebisho madogo ya sheria

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Kilimo imeandaa mapendekezo ya marekebisho madogo (Miscellaneous Amendment) ya Sheria ya Usalama wa Chakula Na.10 ya mwaka 1991, itakayosaidia kusimamia na kuendeleza tasnia ya mazao ya bustani.

Akijibu swali la Mbunge wa Njombe, Deodatus Mwanyika aliyeuliza lini Serikali itaanzisha wakala wa kudhibiti mazao ya mbogamboga na matunda nchini, Naibu Waziri wa Kilimo,  Anthony Mavunde amesema Serikali inajua umuhimu wa mazoa ya bustani na kwamba haitafanya jambo litakalokuwa  mzigo kwa wakulima.

Mavunde amesema muswada huo utapelekwa bungeni baada ya kukamilika na kujiridhisha.

Katika swali la nyongeza, mbunge huyo amehoji Serikali inatarajia kufanya mabadiliko hayo ni lini yatapelekwa bungeni na kama hautakuwa mzigo katika kuongeza kodi na tozo kwa wakulima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live