Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Fedha, TRA waweka mkakati ukusanyaji kodi

9782 Fedha+pic TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, Dotto James amekutana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa wilaya na mkoa kujadili namna ya kukusanya Sh18 trilioni mwaka wa fedha 2018/2019.

Mkakati huo unawekwa wakati taarifa zikionyesha mamlaka hiyo haikufikia lengo la makusanyo ya kodi katika bajeti ya mwaka 2017/18.

Mwaka 2017/18 mamlaka hiyo ililenga kukusanya Sh17.1 trilioni lakini ikafanikiwa kupata Sh15.5 trilioni hivyo kuwa na tofauti ya Sh1.6 trilioni ambayo ni sawa na nakisi ya asilimia 7.5.

Akifungua mkutano huo leo Alhamisi Agosti 2, 2018   James ameikumbusha menejimenti ya TRA kuwa kati ya Sh32 trilioni za bajeti ya Serikali, Sh18 trilioni ni mapato yatokanayo na kodi ambayo inatakiwa kukusanywa na mamlaka hiyo.

“Katika bajeti hii sera za mapato zinalenga kuongeza wigo wa kodi, kuimarisha usimamizi wa vyanzo vilivyopo hususan katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki na hatua nyingine za kiutawala hivyo tunatarajia TRA watazifuata sera hizo na natumaini tutafika na kuvuka lengo,” amesema James.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz