Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mufindi, SSP Anthony Ngwandu amewakata wakazi wa Kata ya Wambi Halmashauri ya Mji Mafinga, kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kukabiliana na wahalifu.
SSP Ngwadu ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu, March 27, 2023, katika ziara yake ya kujitambulisha na kusikiliza kero za wananchi katika Kata ya Wambi iliyofanyika kwenye ofisi za Kata Mtaa wa Luganga, Mjini Mafinga.
Aidha SSP Ngwadu amesema viongozi wa Serikali za Mitaa na kata wanapaswa kushirikiana na Polisi kata kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu ili wananchi waweze kuwa salama na kuendelea na shughuli zao za Maendeleo bila kusumbuliwa na wahalifu Also Read
Mkurugenzi Jatu ashindwa kufika mahakamani, kesi yakwama Kitaifa 39 min ago Waafrika 29 wazama baharini wakitorokea Italia Kimataifa 39 min ago
"Hakuna mhalifu yeyote atakayebaki salama katika Wilaya hii kwani Jeshi la Polisi lipo imara na limejipanga kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu kwa sababu haiwezekani mtu atoke shamba amechoka halafu usiku akae macho kwa ajili ya kuogopa kuibiwa na wahalifu jambo hili halikubaliki hata kidogo," amesema mkuu huyo.
Hata hivyo, Mkuu huyo ameaomba wananchi wa kata hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ikiwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao ili waweze kukamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani hapa, Hassan Kimaro amekemea vitendo vya baadhi ya watu wenye uwezo wa kifedha kuwalaghai watoto wadogo lakini jamii wanalifu mvua macho bila kuchukua hatua yoyote
Amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Jeshi la Polisi wilaya hapa limejipanga kuhakikisha watu wenye tabia kama hizo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Kata ya Wambi, Farida Kalinga, Ezekiel Mgaya wamelishukuru Jeshi la Polisi Wilaya hapa kwa kuona umuhimu wa kutembelea kwenye kata hiyo kwa ajili ya kusikiliza kero zao.