Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wese Dar ahueni, Mtwara, Lindi na Ruvuma kilio, EWURA yatangaza

Chibu.jpeg Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje.

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji Nchini EWURA imetangaza kushuka kwa bei za rejareja za mafuta ya Petrol,Dizell na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es salaam zimepungua kwa Sh 21 Lita petrol na Sh 44 mafuta ya taa huku mafuta ya dizeli yakipanda kwa Sh 13 kwa Lita.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini.

Hata hivyo bei za rejareja za mafuta ya Petroli na Dizeli kwa mikoa ya kusini (MTWARA, LINDI NA RUVUMA) zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa katika toleo la Januari 5,2022,ikisababishwa na kutokuwepo kwa Shehena ya mafuta iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara kwa mwezi Januari.

Katika hatua nyingine Chibulunje amesema kutokana na ufuatiliaji wa mwenendo wa beinza mafuta katika soko la Dunia ,kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa bei za mafutakwa mwezi Machi na Aprili 2022.

Pamoja na hayo ,EWURA inaendelea kufuatilia mwenendo huo kwa karibu ili kuishauri Serikali hatua za kuchukua katika harakati za kupunguza makali ya be za mafuta nchini.

Katika kuhakikisha kunakuwa na ushinda katika Bei zinazoanza kutumika kesho ununuaji wa mafuta kutoka kwenye maghala Sasa kutakuwa na Bei mbili ambazo ni Bei Kokomo ambayo muuzaji hatatakiwa kuzidisha na Bei ya chini ambayo vilevile muuzaji hatakiwi kushuka zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live