Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye viwanda waifagilia bajeti

TYYY.webp Wenye viwanda waifagilia bajeti

Tue, 16 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini (CTI), limepongeza bajeti ya serikali ya mwaka 2020/21 kwani imeyafanyia kazi malalamiko mengi yaliyotolewa na wafanyabiashara na wenye viwanda.

Pongezi hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Msaidizi wa Shirikisho hilo, Paul Makanza, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bajeti hiyo iliyosomwa Juni 11.

Alisema kwenye bajeti hiyo serikali imeondoa mlolongo wa tozo mbalimbali zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara na wenye viwanda hali itakayosaidia kuongeza tija.

Alisema serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuweka mazingira mazuri ya biashara kupitia mpango wake wa Blur Print na imeweka mkakati wa kusisimua biashara na viwanda baada ya kutikiswa na ugonjwa wa corona.

“Serikali imetambua namna biashara na viwanda vilivyoathiriwa na ugonjwa wa corona sasa tunaipongeza kwa kuja na bajeti yenye mwelekeo wa kusisimua uchumi na biashara ziweze kurejea kwenye hali ya kawaida,” alisema Makanza.

Aidha, alisema CTI iko bega kwa bega na serikali kuhakikisha mpango wake wa 2025 unafanikiwa na imeweka mazingira mazuri ili bidhaa nyingi ziongezewe thamani badala ya kuuzwa nje ya nchi zikiwa ghafi.

Makanza alipongeza hatua ya serikali kupunguza kodi ya kujengea uwezo na ujuzi (SDL) kutoka asilimia tano hadi nne na kwamba itasaidia kuongeza ajira na kulinda zile zilizopo.

Alisema sekta ya viwanda imeendelea kukua miaka mitano iliyopita kwani viwanda 8,477 vikubwa, vidogo na vya kati vimejengwa, ambavyo vimesababisha ajira 482,601.

Kuhusu marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao nje ya nchi, alisema ingawa kuna deni kubwa, lakini serikali inajitahidi sana kulipa.

“Viwanda vingi vinavyouza nje havijalipwa ila tunaendelea kuzungumza na serikali kuona namna ya kumaliza deni hilo, lakini tunaona kuna nia ya kulipa kidogo kidogo,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live