Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye amana benki zilizofungiwa wafuate bima TPB

6bea4e9f088b05d1bde439650d6956df Wenye amana benki zilizofungiwa wafuate bima TPB

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANANCHI wote waliokuwa wameweka amana zao katika benki yoyote iliyofungiwa hapa nchini wameombwa kufuatilia fidia ya bima ya amana hizo kwenye tawi lolote la Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa bado hawajafuatilia fidia hizo mpaka sasa.

Kauli hiyo imetolewa jana na kaimu mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana nchini, Richard Malisa katika mafunzo ya siku tano yanayoendelea kwa waandishi wa habari kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu uandishi wa habari za Uchumi, Fedha na Biashara yanayofanyika mkoani Mtwara chini ya Benki Kuu Tanzania (BOT).

Alisema kuwa inapofungwa benki, serikali kwa mujibu wa sheria imeweka utaratibu wa watu kupewa fidia zao kwa utaratibu wa fidia unakuwa watu zaidi ya asilimia 90 wanakuwa hawajapoteza chochote kwenye benki iliyofungwa.

Malisa alisema kuwa fedha ambazo wanatakiwa kulipa fidia hizo ni Sh bilioni 11.52 lakini mpaka sasa wamelipa Sh bilioni 7.3 ikiwa idadi ya watu au wateja wanaotakiwa kulipwa ni 63704 na mpaka sasa tayari waliokwishajitokeza kuchukua fidia zao ni 25,118 ikiwa ni sawa na asilimia 39 tu ya wateja hao waliobaki ni 38,586 na kiasi kilichobaki ni Sh 3,683,617,284.66.

Alisema kuwa wateja hao waliojitokeza kwa sehemu kubwa ni wale ambao wamekuwa na kiwango kikubwa cha fedha lakini wengi bado labda wanashindwa kufuatilia kwa kuhofia gharama za ufuatiliaji ikilinganishwa na kiasi cha fedha zao na wengine inawezekana bado hawajapa habari kuwa, benki inapofungwa kuna utaratibu wa kupata fidia.

“Kwa hiyo nashukuru leo nimepata fursa hii adimu ya kukutana na wanahabari kwamba mtusaidie kufikisha habari hizi kwa Watanzania wafahamu kuwa benki inapofungwa kuna utaratibu wa kupata fidia kwa kila mtu anayestahili kupata fidia,” alisema Malisa.

Bodi hiyo inayowajibu wa kuuza mali kwa benki iliyofungiwa ili kinachopatikana wanagaiwa wale ambao walikuwa wanaidai benki husika kwa hiyo ndiyo maana ya ufilisi na kinachofanyika kwa sasa ni kukusanya mali zote za benki hizo na kuziuza katika utaratibu unaokubalika wa sheria ili warudishe fedha za zinazodaiwa na wananchi hao.

Chanzo: habarileo.co.tz