Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wengi hawatumii gesi kwa kuogopa mitungi kulipuka

GESII WEBB Wengi hawatumii gesi kwa kuogopa mitungi kulipuka

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pamoja na jitihada zinazofanyika ili watu wengi wahamie katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi, uoga wa mitungi kulipuka imetajwa kuwa moja ya kikwazo.

Hofu hii inatajwa sasa ikiwa ni baada ya gharama ya upatikanaji wa nishati hiyo kuwa kilio cha muda mrefu

Hayo yamesemwa leo Machi 9 wakati wa kutangaza kongamano la siku tatu la kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia linalotarajia kukutanisha zaidi ya kampuni 50 zinazozalisha gesi ya kupikia na vifaa vyake kutoka nchi tofauti duniani ndani ya jiji la Dar es Salaam.

“Kuna wengine hawatumii gesi si kwa sababu hawana uwezo, wengine wanaogopa kuwa inaweza kulipuka, watakuambia dada hajui namna ya kutumia vizuri, hataifunga vizuri, nafikiri tuna kazi kubwa sana ya kuelimisha kuhusu matumizi ya gesi na manufaa yake,” amesema Amos Jackson ambaye Mkurugenzi mtendaji wa Tanzania LPG Association.

Amesema suala hilo limekuwa ni moja ya kikwazo katika ufanikishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na hadi sasa asilimia 63.5 ya Watanzania bado wanatumia kuni na asilimia 24 wakiwa wanatumia mkaa.

Mbali na hilo amesema ni vyema kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa gesi ya kupikia ili kuwapunguzia watanzania gharama za mara kwa mara.

Hiyo ni kutokana na kile alichoeleza kuwa wakati mwingine, kampuni huingia katika soko na kupotea ndani ya muda mfupi huku ikiwaacha watu na mitungi ya gesi ambayo haiwezi kutumika.

“Hii ni gharama, wakati jitihada nyingine zikifanywa na makampuni yanayouza gesi kwa kuwawezesha wateja kulipa kidogokidogo lazima tuhakikisha upatikanaji wake.

Mkurugenzi wa LPG Expo, Catherine Ho amesema mbali na kampuni zinazozalisha gesi kutoka nchi tofauti kushiriki mkutano huo pia baadhi ya wadau kutoka nchi tofauti wamealikwa.

“Mkutano huu unalenga kuweka mazungumzo ya pamoja baina ya Sekta binafsi na Serikali pia wataalamu wanaokuja watafanya utafiti na kutoa suluhisho au ushirikiano kwa Watanzania, hii itaongeza ushindani pia katika sekta,”

Amesema gesi ya kupikia ni muhimu katika nchini zinazoendelea kwa sababu wanawake wamekuwa wakihangaika na matatizo ya kiafya kwa sababu ya matumizi ya njia za kupikia zisizokuwa salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live