Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wekezeni kwenye miradi ya kuzalisha ajira

Ajira Mpyaaaaa Wekezeni kwenye miradi ya kuzalisha ajira

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameelekeza Menejimenti ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji ili kuchochea uchumi na fursa za ajira nchini.

Mhandisi Luhemeja amesema hayo, alipofanya ziara ya kiutendaji katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya PSSSF, jijini Dar es Salaam, ambapo, pamoja na kujionea shughuli za utoaji huduma, pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimengti ya Mfuko huo ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, CPA. Hosea Kashimba. “Kuna kundi la vijana, kundi ambalo halina matumaini, zamani wahitimu wa Chuo Kikuu walikutana na ajira, lakini sasa hivi hali hiyo ni tofauti kidogo.” Alifafanua.

Alisema PSSSF ni Mfuko mkubwa hivyo una jukumu la kuwasaidia Wastaafu, lakini pia kujenga mazingira ya kuwawezesha wastaafu wengi siku za usoni. “Fungueni viwanda vingi, vitasaidia kutengeneza ajira kwa vijana, unaposaidia watu wengi na wewe unajisaidia.” Alifafanua.

Pia ameelekeza Menejimenti ya PSSSF, kuendelea kutoa elimu kwa umma, ili Wananchi waweze kufahamu kazi kubwa ambayo imefanyika toka kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, GEPF na LAPF na kuanzishwa PSSSF. “Kazi kubwa na nzuri imefanyika kwa kipindi cha miaka mitano toka kuunganishwa kwa Mifuko hiyo, utendaji umeboreshwa kwa kiasi kikubwa, ni muhimu watanzania waweze kuelewa kazi ambayo Serikali inafanya kwa niaba yao” alisema Mhandisi Luhemeja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, amesema, yeye na Menejimenti yake kwa ujumla wameyapokea maelekezo hayo na ameahidi kuyafanyia kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live