Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wekeza hivi kwenye kampuni kibiashara

Fedhapic Wekeza hivi kwenye kampuni kibiashara

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna fursa nyingi za uwekezaji. Lakini pia unapowekeza kwa namna yoyote ile matokeo mawili ni muhimu, ambayo ni kupata ama kupoteza. Hii ni kwa uwekezaji wa namna yoyote ile, uwe ni kwenye biashara, kilimo, mifugo au uwekezaji wa kwenye ardhi. Pia iwe ni kwenye biashara ndogo au kubwa.

Kwa mwekezaji wa kawaida (ambaye anataka kuwekeza hata shilingi elfu tano tu) anaweza kuona pengine fursa nzuri zaidi ya kupata rejesho kwa kile anachoweza kuwekeza ni kumiliki sehemu ya kampuni ambazo tayari zimekwisha jiimarisha kibiashara.

Mara nyingi ni kampuni zinazojishughulisha na kuuza bidhaa ama kutoa huduma ambazo zinatumika na watu wengi.

Zipo zinazojihusisha na kutoa huduma ama kutengeneza bidhaa ambazo zinatakiwa kila siku na walaji, inaweza kuwa fursa nzuri ya kujihusisha kuwekeza na kupata rejesho kwa mtaji ambao unapanga kuwekeza.

Kwa mfano, uwekezaji kwenye kampuni ya maji, umeme, simu, benki, vyakula, intaneti, usafirishaji, ama madawa – kuna uhakika wa kupata marejesho kwa sababu makampuni haya kutokana na jinsi yatakavyoshindana kwenye soko, yanaweza kupata faida na kutoa gawio kwa wanahisa wake.

Baadhi ya makampuni haya yanaweza kuwa makubwa sana kiasi kuwa ukosekanaji wa huduma ama bidhaa zake unaweza kuathiri uchumi, na hivyo basi yanakuwa si rahisi sana kufilisika kama makampuni madogo.

Kampuni nyingi ambazo pengine mwekezaji mdogo angependa kushiriki ni za binafsi ama zinamilikiwa na serikali au mashirika ya kiserikali na hivyo si rahisi kwa mwekezaji ambaye si mwanahisa ama serikali aweze kufikiria kumiliki kampuni hizo. Kampuni nyingine za namna hii zinaweza kuwa ni za nje na hivyo zinamilikiwa na wawekezaji wa nje.

Faida ya kuwekeza kwenye kampuni hizi ni kuwa zina mifumo imara ya usimamizi wa biashara na fedha, zina uhakika wa biashara na hivyo si rahisi kupata hasara, ambapo kuwa uwezekano mkubwa pia wa kupata gawio.

Hata hivyo, kuna namna ambavyo mtu binafsi anaweza kushiriki kuwa mmojawapo wa wawekezaji kwa baadhi ya kampuni hizo kupitia masoko ya hisa na mitaji kama Soko la Hisa la Dar es Salaam, ama kupitia uwekezaji wa hati fungani za serikali ama za mashirika binafsi, au kupitia uwekezaji wa makampuni yanayojihusisha na uwekezaji kupitia hazina maalumu ya pamoja (mutual funds), uwekezaji kupitia taasisi za kifedha za kitengo maalum cha vipimo (Unit Trust) ama uwekezaji wa jumla (collective investment schemes).

Uwekezaji kupitia njia hizi unarahisisha mambo mengi ambayo mwekezaji anaweza kuyafaidi, ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwa usalama. Hii ni pamoja na kujihakikishia unawekeza kwenye kampuni ama shirika lililosajiliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Soko la Hisa na Mitaji.

Mwekezaji pia ana uwezo wa kupanga malengo yake ya uwekezaji, na inatoa fursa ya kuuza hisa ama dhamana na kupata fedha taslimu pale malengo yako ya uwekezaji yanapotimia ama kubadili mwelekeo wako wa uwekezaji.

Ni vizuri kujua kuwa uwekezaji kwenye makampuni si kuwa ni lazima kupata gawio, lakini yana usalama zaidi kwenye uwekezaji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live