Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa biashara Zanzibar, afafanua unafuu wa kodi za bidhaa zinazofikia visiwani humo

Kodi Magari Waziri wa Biashara Zanzibar, afafanua unafuu wa kodi za bidhaa.

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda visiwani Zanzibar, Omar Said Shaaban, ametoa ufafanuzi kuhusu suala la kodi za biadhaa zinazotozwa visiwani humo kutofautiana na ile ya bara, kuwa kilichopo ni unafuu wa kodi wa takribani 40% kwa bidhaa zinazofikia visiwani humo.

Amesema kuwa, inapotokea mtu kusafirisha bidhaa kutoka visiwani humo kuja bara itambidi kulipa kodi iliyopungua ili afanane nayule aliyeshusha mzigo wake moja kwa moja bara.

"Mtu anapoagiza Gari na kulishushia Zanzibar kwa matumizi ya Zanzibar huwa kuna unafuu wa Kodi 40% (kama Kodi ni Milioni 1 utalipa Laki 4 au 6), ila kama Gari lile utalisafirisha Bara watakutoza ule utofauti ili ufanane na mwenzie aliyeshushia Gari Bara moja kwa moja ili mlipe Kodi sawa ya Milioni 1" - Waziri wa biashara Omar Said Shaaban, Waziri wa biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live