Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Nishati Uganda apigilia msumari mradi wa EACOP

Bomba La Mafuta Msh Waziri wa Nishati Uganda apigilia msumari mradi wa EACOP

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati na Mandeleo ya Madini wa Uganda, Dkt. Ruth Nankabirwa, amesema kuwa Tanzania na Uganda zinaendelea kushirikiana kusimamia mradi wa Bomba la Afrika Mashariki (EACOP) ili kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania kwa maslahi ya wananchi wa mataifa hayo na Afrika Mashariki kwa ujumla

Amesema hayo wakati wa sherehe za uzinduzi wa kiwanda cha kuweka mfumo wa upashaji na kutunza joto kwenye vipande vya mabomba ya kusafirisha mafuta hayo kwenda nje kupitia Tanzania. Amesema kati ya visima 426 tayari visima 26 vimechimbwa nchini Uganda na kasi ya uchimbaji inaendelea vizuri ili kupata mafuta ya kutosha.

"Nawaomba wadau na washirika wote wa mradi huu waendelee kushirikiana na kuweka nguvu kufikia malengo. EACOP wamepokea vibali kutoka Uganda na Tanzania, hivyo tumefika hatua ambayo hatuwezi kurudi nyuma," amesisitiza Dkt. Nankabelwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live