Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Mifugo aagiza kuondolewa msimamizi wa mnada Pugu

8287cabc86a0063acb4bba82a6bb5e8c Waziri wa Mifugo aagiza kuondolewa msimamizi wa mnada Pugu

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi na Uvuvi, Mashimba Ndaki amemtaka Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Nyangogo Justine kumuondoa katika usimamizi wa mnada, Sajenti Ahmad na wenzake waliokuwa zamu jana Machi 9, 2021 kwa tuhuma za kutoa taarifa zisizo sahihi za idadi ya mifugo inayoingia mnadani.

Ndaki amesema hayo leo Machi 3,2021 jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea mnada wa Pugu kukagua namna watumishi wa umma wanaofanya kazi katika mnada huo wanavyohakikisha wanasimamia vyema mapato ya serikali.

Mara baada ya kukagua vitabu vya taarifa za mifugo katika mnada huo, waziri huyo alibaini dosari katika taarifa za Kikosi Maalum cha Kuzuia Wizi wa Mifugo.

Kufuatia hali hiyo, waziri huyo amemtaka Mkuu wa Mnada wa Pugu, Kerambo Samwel na viongozi wengine wa mnada katika vitengo mbalimbali kuhakikisha wanatunza vyema kumbukumbu za shughuli za mnada na kufanya kazi kwa uadilifu.

Aidha alisema lengo la serikali ni kukusanya zaidi ya bilioni tatu kupitia mnada huo mpaka kufikia Juni 30,2021 licha ya changamoto mbali mbali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz