Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri atoa onyo kwa wababaishaji

11133 Waziri+pic.png TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh amesema wizara hiyo haitawaonea aibu wafanyabiashara watakaokwenda kinyume na matakwa ya sheria ya uendeshaji biashara.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa baraza la biashara kwa vijana wa mkoa wa Mjini Magharibi, lenye lengo la kuwainua zaidi vijana.

Hafidh pia alibainisha kuwa ipo haja ya vijana kuendelezwa kiuchumi lakini watalazimika kufuata sheria na taratibu za Serikali.

“Naamini uanzishwaji wa baraza hili la biashara kwa vijana utakuwa chachu ya kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara,” alisema.

Naye mwenyekiti wa baraza hilo, Ayoub Mohamed Mahmoud ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi alisema watatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria kwa kushirikiana na baraza la biashara la taifa ili kuondoa kasoro zilizopo.

Chanzo: mwananchi.co.tz