Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri atoa msimamo mradi wa gari za umeme mlima Kilimanjaro

61896 Mlima++pic%255C

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis  Kigwangalla amewaondoa hofu waongoza watalii na wapagazi juu ya mradi wa kutumia gari maalumu za umeme (Cable Car) kupandisha watalii Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa waongoza watalii bora Jumamosi, Juni 8, 2019, Waziri Kigwangalla alisema kabla ya mradi huo kuanza, wadau watashirikishwa.

Alisema mradi huo utakuwa na lengo la kusaidia makundi maalumu kama walemavu kukaribia kuona kilele cha mlima huo na kamwe haitarajiwi kuondoa ajira kwa vijana au kuharibu ikolojia ya mlima huo.

"Hii ni products (bidhaa) mpya katika kuongeza watalii kupanda mlima Kilimanjaro lakini haitavuruga utaratibu wa watalii kupanda mlima kwa kutembea," alisema

Awali, mwenyekiti wa tuzo wa waongoza bora wa watalii, Christopher Nzela aliomba kuitishwa kikao maalumu cha ufafanuzi wa jambo hili kwa sababu linawapa hofu.

Alisema kuna taharuki kuwa mradi huo unakwenda kuondoa ajira kwa Watanzania wengi pamoja na biashara ya utalii ndiyo sababu wanataka kushirikishwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz