Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri ataka majibu soda kupanda bei

Soda Baadhi ya vinywaji baridi

Tue, 18 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaju ameitaka tume ya ushindani nchini, FCC kutoa ripoti kwa Serikali ikieleza kwanini Vinywaji baridi na Vifaa vya ujenzi vimepanda bei.

Dkt.Kijaji amehoji tume hiyo ni tafiti zipi wanazozifanya ili kudhibiti hali ya mfumuko holela wa bidhaa.

"Ni vipi tunasubiri mwezi mzima vinywaji baridi kama soda zinapotea, zinapoteaa kisha wafanyabiashara wanapandisha bei halafu ndio tunakuja? kwa hili hapana na ninaagiza ndani ya siku tatu nipate majibu kwanini vinywaji baridi vimepotea ndani ya soko la taifa letu na nini kimesababisha na tunatokaje hapa tulipo na kwanini bei inapanda? tuwape majibu watanzania" alisema Kijaju

Katika hatua nyingine Dkt.Kijaji ametoa siku 7 kupata majibu kwa nini kumekua na ongezeko la kupanda bei kwa vifaa mbali mbali vya ujenzi .

Tangu mwishoni mwa mwaka jana, katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuli ripotiwa kupanda kwa bei kiholela kwa bidhaa tajwa zikianzia na saruji kisha vinywaji baridi kwa mwezi desemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live