Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri ataja chanzo kudorora ufugaji

Mifugo Mnadani Waziri ataja chanzo kudorora ufugaji

Thu, 10 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk. Khalid Salum Mohamed, alisema jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Mfenesini, Machano Othman Said.

Katika swali hilo, Machano alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuimarisha sekta ya mifugo na kuzalisha maziwa.

Alisema sababu zilizofanya kuyumba kwa sekta hiyo ni kukosekana kwa maeneo ya malisho ya mifugo kutokana na maeneo mengi sasa kutumika kwa shughuli za ujenzi wa nyumba za kudumu.

Waziri alitaja sababu nyingine kuwa ni ukosefu wa mbegu bora kwa wafugaji wa ng’ombe wa kisasa ambao ni maarufu kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa.

Pia alisema wizi wa mifugo ni miongoni mwa changamoto iliyojitokeza hivi karibuni hatua ambayo imesababisha wafugaji wengi kuanza kukata tamaa na maendeleo ya sekta hiyo.

Aliyataja maeneo ya Wilaya ya Magharibi A Unguja, ambayo awali yalikuwa yakitumika kwa ajili ya malisho ya wanyama kuwa  hivi sasa yamegeuzwa kwa ajili ya matumizi ya makazi ya kudumu.

“Mheshimiwa Spika, napenda kuwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba ni kweli sekta ya ufugaji hivi sasa imeyumba sana kutokana na maeneo mengi ya malisho kutumika kwa shughuli za ujenzi wa nyumba za kudumu''alisema.

Aliitaja mikakati ya baadaye ya serikali kuwa ni kujenga kiwanda cha malisho ya chakula cha mifugo ambacho kwa kiasi kikubwa kitaimarisha sekta ya ufugaji.

Chanzo: ippmedia.com