Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri apiga ‘stop’ mgodi kuuzwa

49851 Pic+biteko Waziri apiga ‘stop’ mgodi kuuzwa

Mon, 6 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa madini Dotto Biteko, amesikitishwa na kitendo cha uongozi wa mgodi wa madini ya almasi Mwadui (Wiliamson Diamond), uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kutaka kuuzwa kienyeji bila serikali kupewa taarifa.

Pia alisema sababu ambazo wanazitoa mgodi huo za kusitisha shughuli za uzalishaji na kutaka kuuza, kutokana na kushuka kwa bei ya almasi duniani sababu ya corona haina mashiko, bali wawe wakweli kama wamefilisika.

Kwa upande wake meneja mkuu wa mgodi huo, Ayoub Mwenda, alikiri hawakutoa taarifa serikalini juu ya kutaka kuuzwa kwa mgodi huo, huku wakiahidi kufuata maelekezo yote ambayo yametolewa na Waziri wa Madini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, aliipongeza serikali kwa kuisimamia vizuri sekta ya madini, kwa kuondoa migogoro pamoja na kupigania rasilimali za Watanzania na kuinua uchumi wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live