Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri: Wafanyabiashara heshimu sheria

Kijajipic Data Waziri: Wafanyabiashara heshimu sheria

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amewataka Wafanyabiashara nchini kuheshimu sheria za ndani na nje ya nchi ili wasipate changamoto katika usafirishaji wa bidhaa.

Dkt. Kijaji amezungumza hayo baada ya kuwepo kwa sintofahamu kwa Wafanyabiashara wa Mahindi waliozuiwa mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Amewataka Wafanyabiashara kuhakikisha wanafahamu sheria hasa wanapokwenda kununua ama kupeleka bidhaa nchi jirani.

"Nimesikia na leo wamezuiwa katika mpaka wa Malawi, niwasihi Wafanyabiashara kufahamu sheria kabla ya kwenda kununua ama kuuza bidhaa nchi jirani"- ameongeza Dkt. Kijaji

Chanzo: www.tanzaniaweb.live