Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy akoshwa na ushiriki wa TMDA maonesho ya Sabasaba

WhatsApp Image 2022 07 08 At 1.jpeg Waziri Ummy akoshwa na ushiriki wa TMDA maonesho ya Sabasaba

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam ambapo amefurahiswa na Mamlaka hiyo kushiriki maonesho hayo.

Amefurahiswa na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu ubora , usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa,vifaa tiba pamoja na vitendanishi lakini kubwa zaidi ambalo Waziri wa Afya ni baada ya kuona namna gani wanatoa elimu kuhusiana na madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa za tumbaku.

Kingine ambacho Waziri Ummy Mwalimu amefurahiswa ni kuona TMDA inajipanga katika kuhakikisha masuala mazima ya kutoa elimu hususani katika kueleza kemikali ambazo zipo katika bidhaa za tumbaku na katika kuelezea wamekuwa wakionesha kemikali za sumu ambazo zinapatikana kwenye tumbaku.

Hivyo amefurahi kuona Wananchi wanapata uelewa kwasababu suala zima la matumizi ya tumbaku linahitaji mtu awe na uelewa anapoingia katika matumizi yale ajue kabisa nini matokeo yake.

Akiwa katika banda hilo, maofisa wa TMDA wakiongozwa na Mkurugenzi wao Adam Fimbo wamemueleza Waziri kuwa wamekuwa wanahusisha wadau ambao wanamiliki maeneo ya wazi kuzingatia yale yanayotakiwa kufanyika kwa maana ya kutenga eneo maalum ya uvutaji lakini waweke alama za kuonesha No Smoking na Smoking area.

Lengo la kufanya hivyo ni kumkinga asiyetumia na wanaotumia wajue nini kitatokea kutokana na matumizi ya tumbaku.Waziri Ummy ambaye alikuwa ameambatana na Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa Dk .Ted Chaiban ambapo naye ameonesha kufurahia hatua zinazochukuliwa na TMDA katika kuelimisha umma kuhusu usalama na ubora wa dawa na vifaa tiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live