Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ulega awataka Watanzania kuwekeza katika sekta ya uvuvi kunalipa

Waziri Ulega Awataka Watanzania Kuwekeza Katika Sekta Ya Uvuvi Kunalipa.jpeg Waziri Ulega awataka Watanzania kuwekeza katika sekta ya uvuvi kunalipa

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kuwa serikali imewekza katika sekta hiyo hivyo watanzania watumie fursa ya ufugaji na Uvuvi kutokana kuwepo kwa soko la uhakika.

Ulega aliyasema hayo kwenye la Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ulega amesema kuwa sekta ya mifugo ya Uvuvi kuachana na biashara mazao yake kwa kula na kunywa ndio yanafanya kujenga afya.

Ulega amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imefungua mipaka hivyo kwa watanzania wanauhakika wa masoko ya ndani pamoja na masoko nje kuuza bidhaa zitotokanazo na Mifugo pamoja na Uvuvi.

Aidha amesema kuwa serikalo inatarajia kujenga miundombinu itayofanya ya kuvuta samaki ambayo mvuvi hana sababu ya kwenda mbali kutafuta samaki.

Ulega amesema kuwa ufugaji na Uvuvi kwa sasa unakwenda kisasa kutokana kuwepo watalaam ambao wanashauri na kuweza kufanya mtu kunufaika na kile anachofanya kwa kumpa faida zaidi ya mara mbili.

Waziri huyo amesema maonesho ya sabasaba wananchi wafike katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo watajifunza ufugaji na uvuvi wa kisasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live