Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ulega ataka wazalishaji mazao ya mifugo kutumia teknolojia

Ulega Pic Data Waziri Ulega ataka wazalishaji mazao ya mifugo kutumia teknolojia

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amewataka wafugaji na wazalishaji wa mazao ya mifugo na uvuvi kuwekeza katika teknolojia za kisasa na vitendea kazi sahihi vitakavyongeza uzalishaji wa mifugo na uvuvi.

Ulega ameyasema hayo jijini Arusha leo Jumatano Oktoba 25, 2023 wakati akifungua kongamano la 46 la chama cha wazalishaji na wataalamu wa mifugo na uvuvi Tanzania (TSAP).

Amesema Wizara itahakikisha inaweka mazingira bora ya kufuga, kusindika na kufanya biashara ya mazao yatokanayo na mifugo ma uvuvi na makundi yote katika mnyororo mzima wa thamani.

“Ni wakati muafaka wa kufanya mapinduzi katika mnyororo mzima wa tha-mani ya mifugo na samaki ili kukidhi mahitaji ya chakula na lishe bora kwa wananchi na masoko yanayotuzunguka,” amesema Ulega

Amefafanua kuwa wizara inatilia mkazo katika uwekezaji wa malisho na mbegu kwani kuna uhitaji mkubwa wa rasilimali hizo ikiwemi vyakula bora vya mifugo na samaki, vifaranga bora wa kuku, nyama bora ya ng'ombe, maziwa na bidhaa zake. “Sekta za mifugo na uvuvi zinatazamwa kama ni sekta ndogo na kinachosabisha kujidogosha ni sisi wenyewe na hatuta faulu bila kuweka msitari utakaotuongoza hivyo naelekeza kuanzishwe kwa tasisi imara itay-osimamia hizi tasisi za mifugo ma uvuvi,” amesema Amesema serikali inaendelea kuweka mkakati imara wa kuwashirikisha vijana wasomi katika programu ya BBT ili kuongeza tija katika mifugo na uvuvi.

Mwenyekiti wa TSAP, Dk Jonas Kizima amesema kwasasa chama hicho kina wanachama 300 na kinaundwa na wataalamu wa mifugo na uvuvi Bara na Visiwani Zanzibar lengo likiwa ni kuhimiza maendeleo katika sayansi ya mifu-go na uvuvi lakini pia kushirikiana na wataalamu wa sekta zote.

Dk Kizima ameeleza kuwa katika mkutano huo wa siku tatu wataweza kuwasilisha makala 36 za kisayansi ikiwa ni pamoja na mada mbili za kitaifa na ku-jadiliwa na wanachama wote.

Mtendaji Mkuu wa chama hicho, George Msalia amesema kama wataalamu wanataka kutoa mchango kwa sekta hizo mbili ili ziendelee kutoa mchango katika uchumi wa nchi.

“Sisi ndio wataalamu tunaofanya kazi na wafugaji na wavuvi lakini pia na wa-tu wanaofuga samaki, tunawapa ushauri mbalimbali na tunakutana mara moja kwa mwaka kuzungumza habari za kisekta, kuangalia tulikitoka na tuko-kwenda, tuna changamoto gani na wapi tuendelee kujipanga,”amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live