Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ulega akabidhi boti za uvuvi Mkuranga

Waziri Ulega Akabidhi Boti Za Uvuvi Mkuranga Waziri Ulega akabidhi boti za uvuvi Mkuranga

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika jitihada za kuinua uchumi wa bluu nchini, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega amekabidhi boti 8 za uvivu kwa vikundi vya akina mama,vijana na watu binafsi zitakazo saidia kuinua uchumi wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi boti hizo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo katika kata ya Kisiju, wilayani Mkuranga mkoani pwani Oktoba 9, 2023, waziri ulega ametoa rai kwa wanufaika wa boti hizo kuzitunza na kuzitumia vyema ili waweze kuboresha shughuli zao.

Aidha ameongeza kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa ubunifu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuinua maisha ya wananchi kwa vitendo.

Boti hizo 8 alizozigawa Waziri Ulega ni miongoni mwa boti 168 zenye thamani ya bilion 11.6 ambazo zimetolewa na Rais, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan nchi nzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live