Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Tax aitaka JKT kuzalisha mafuta ya kupikia kwa wingi

Mafuta Pic Waziri Tax aitaka JKT kuzalisha mafuta ya kupikia kwa wingi

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) Dk Stergomena Tax amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi Kujenga Taifa (Suma-JKT), kujikita katika kilimo alizeti ili kukabiliana na uhaba wa mafuta ya kupikia unaojitokeza mara kwa mara. Dk Tax ameeleza hayo jana Julai Mosi, 2022 wakati kuadhimisha miaka 41 ya kuanzishwa kwa Suma -JKT. Halfa hiyo ilihudhuriwa pia na mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi nchini (CDF), Jenerali Jacob Mkunda. Halfa hiyo iliyohudhuriwa pia na mameja jenerali, manadhimu na viongozi wa jeshi hilo wastaafu waliohudumu JKT, ilikwenda sambamba na uzinduzi wa kitabu cha JKT kinachoeleza shughuli mbalimbali zilizofanywa na Suma -JKT tangu kuanzishwa Julai Mosi 1981. Kwa nyakati tofauti wananchi wamekuwa wakikumbana uhaba mafuta ya kupikia kwa sababu mbalimbali ongezeko la bei ya mafuta hayo katika masoko ya kimataifa na gharama za uzalishaji kwa wazalishaji wa ndani ni sababu ya kuadimika kwa bidhaa. Ndio maana Juni mwaka jana aliyekuwa waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda alisema SerikalI itasambaza mbegu za alizeti katika vyama vyote vya ushirika na kuziwezesha kampuni kubwa za uchakataji kuongeza uzalishaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live