Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri: Tanzania inaongoza kwa watalii Afrika

Utaliii Afrika Tz Tanzania inaongoza kwa watalii Afrika

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana leo Bungeni Dodoma amesema "Kufuatia jitihada za Wizara za kutangaza vivutio kwenye masoko mbalimbali na kuboresha huduma za utalii na uhifadhi, Tanzania imeendelea kutambulika kimataifa na kupata tuzo mbalimbali zikiwemo, Hifadhi ya Taifa Serengeti kuwa hifadhi inayoongoza kwa ubora Barani Afrika kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021"

"Pia Tanzania imekuwa nchi inayoongoza kwa shughuli za utalii Barani Afrika, tuzo hizi zilitolewa na World Travel Award, tuzo nyingine ni pamoja na Travellers’ Choice Destination – National Parks of the World, iliyotolewa na Tripadvisor ambapo Tanzania imeingiza hifadhi nne (4) katika orodha ya hifadhi 25 bora duniani zikiongozwa na Hifadhi ya Taifa Serengeti"

"Hifadhi nyingine ni Hifadhi za Taifa Kilimanjaro na Tarangire na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, vilevile, Shirika la Hifadhi za Taifa limetunukiwa Cheti cha Ubora wa Huduma za Kiwango cha Kimataifa cha ISO 9001:2015 kutokana na kuimarishwa kwa utoaji wa huduma bora za utalii"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live