Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mwijage atoa neno bei ya saruji

14147 Waziri+pic TanzaniaWeb

Tue, 28 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Serikali haipangi bei ya saruji badala yake wazalishaji wafuatilie bei hadi kwa mnunuzi wa mwisho.

Mwijage amesema hayo leo Agosti 27, 2018 mara baada ya kufanya ziara kwenye viwanda vya kuzalisha saruji vya Camel na Twiga jijini Dar es Salaam. Kauli ya Mwijage imekuja siku kadhaa baada ya kupanda ghafla kwa bei ya saruji hapa nchini.

Amesema mchezo mchafu wa kupandisha bei ya saruji kiholela unafanywa na wauzaji wa jumla na kusababisha kadhia kwa wananchi.

"Kuna wauzaji wa jumla nitawanyang'anya leseni kwa sababu ninajua mchezo wanaofanya.”

"Simamieni hadi mwisho kujua bidhaa zenu zinauzwa kulingana na bei husika, badala ya kuwaacha wafanye wanavyotaka, ninawajua na nitaambatana nao,” amesema Mwijage.

Mwijage amesema saruji inapokosekana wenye viwanda kama wameshindwa kuendesha biashara yao anawafungia mawakala wasio waaminifu.

Kwa upande wake, mkurugenzi msaidizi wa kiwanda cha saruji cha Camel, Ghalib Ghalib amesema changamoto wanazokutana nazo na kuchangia kupunguza uzalishaji ni ukosefu wa umeme na malighafi ya kuzalishia bidhaa hiyo.

"Kwa kawaida tunazalisha tani 600 kwa siku, lakini tatizo la umeme na malighafi itasababisha tupunguze na kuzalisha tani 400 hadi 500 kwa siku," amesema 

"Hatujatoka nje ya Dar es Salaam, soko letu ni hapa Mbagala pekee," ameongeza Ghalib.

Naye meneja masoko wa kiwanda cha Twiga, Danford Semwenda amesema wao kama kiwanda hawajawahi kupandisha bei.

Amesema siku zilizopita walipunguza uzalishaji kwa asilimia 25 kwa sababu walikuwa wanafanya matengenezo ya kawaida ya mitambo yao ambayo hufanyika kila mwaka.

"Tutayafanyia kazi maelekezo hususani ya kuwafuatilia wasambazaji wetu,’’ amesema Semwenda.

Chanzo: mwananchi.co.tz