Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mwijage: Ni aibu kuagiza pipi kutoka nje

15449 Mwijage TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Magu. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya kuhimili ushindani kwenye soko la ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la Isangijo wilayani Magu leo Septemba 4, 2018, Waziri Mwijage pia amewataka wawekezaji wa ndani kuzalisha bidhaa zinazotumika kwa wingi nchini na kuliondolea Taifa aibu ya kuagiza hadi pipi kutoka nchi ya nchi.

"Ilikuwa ni aibu Taifa kuagiza nje hata pipi; kiwanda kama hiki kinachozalisha pipi na bazoka (jojo) ni ukombozi si tu kwa fursa za ajira na kodi, bali pia kwa kuondoa aibu ya kuagiza pipi nje," amesema Mwijage.

Amesema ni aibu ya kuagiza pipi kutoka nchi za China, Kenya na mataifa mengine ya Asia, aibu ambayo sasa imeanza kuondoka.

Mkurugenzi wa kiwanda cha Lakairo, Dan Lakairo amesema kiwanda hicho kilichotoa ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 400 pia kinatengeneza vishangishio na steel wire.

Chanzo: mwananchi.co.tz