Menu ›
Biashara
Thu, 15 Jun 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, amesema Serikali ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni.
Mwigulu ameyasema hayo mapema leo Juni 15, 2023, bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka wa Fedha 2023-24.
“Hadi kufikia Aprili 2023 akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani bilioni 4.88 ambayo inatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takriban miezi 4.4. Mahitaji ya nchi kisheria ni kuwa na kiasi kinachotosheleza muda usiopungua miezi 4,” alisema Mwigulu Nchemba.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live