Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu kazungumza kuhusu Watanzania kuitumia Posta

Kassim Majaliwa 12posta Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ametoa rai kwa Watanzania kutumia huduma za shirika la posta nchini hususani katika usafirishaji wa vifurushi (Mizigo ama Bidhaa), ili kukuza uchumi wa nchini.

Ameyasema hayo akiwa katika Hafla ya Uzinduzi wa Shirika hilo, uliohudhuriwa na viongozi wa ngazi ya Mkoa jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Jiji humo, Amos Makalla pamoja na Wakuu wa Wilaya.

Ametolea mifano ya baadhi ya mashirika ya posta kutoka nchi za nje yanavyofanya kazi hapa nchini kwa ushindani hivyo kuwataka Watanzania kutumia shirika lao la posta kwani sasa ni la kidigtal zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live