Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu awataka mabalozi kuvutia wawekezaji

7d6eb5f7eb08b0d8d8788c1ec0ce978b Waziri Mkuu wa Tanzania akizungumza na Mabalozi wateule mapema hii leo

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa kuhamasisha uwekezaji.

Majaliwa amekutana na mabalozi hao leo (Jumatatu, Januari 17, 2022) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma. Mabalozi aliyokutana nao ni Balozi Profesa Adelardus Kilangi (Brazil), Balozi Said Juma Mshana (DR-Congo), Balozi Alex Gabriel Kalua (Israel), Balozi Said Shaib Mussa (Kuwait) na Balozi Fredrick Ibrahim Kibuta (Urusi).

Aidha amewataka mabalozi hao wahakikishe wanakwenda kupunguza gharama za uendeshaji wa balozi kwa kubana matumizi hususani katika mambo yasiyokuwa ya lazima. “Pia mkaimarishe mahusiano kati yenu na maafisa wa ubalozi.”

Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao wakutane na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) na wawasaidie kuimarisha Jumuiya zao kwa kuwa na uongozi imara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live