Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maboresho makubwa yanayofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ya kujenga maeneo ya kuhifadhi mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoharibika kwa haraka ni muhimu na inahitaji utekelezaji wa haraka hasa katika kipindi hiki ambacho sekta binafsi inakaribishwa kufanya kazi katika bandari.
Waziri Mkuu ameyasema hayo mkoani Mbeya alipotembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ya Kimataifa ya Nanenane.
Ameitaka TPA kuharakisha taratibu zote za ujenzi wa eneo la kuhifadhia mazao hayo ili kufanikisha usafirishaji wa mazao nje ya nchi.
Eneo hilo la kuhifadhi mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoharibika kwa haraka lipo Kurasini, Dar es Salaam ambapo awali lilikuwa likimilikiwa na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA)