Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu ataka sheria ziboreshe uwekezaji

Majaliwa Wadau Waziri Mkuu ataka sheria ziboreshe uwekezaji

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha sheria mpya zinzoundwa na mamlaka hizo zinawezesha mazingira bora ya uwekezaji na biashara nchini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara ya Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji Nchini inayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City

Aidha amezitaka mamlaka hizo kutoa huduma kwa haraka kwa wawekezaji kwa kuweka mifumo itakayowezesha kuwasiliana na wawekezaji kirahisi pamoja na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha shughuli za uwekezaji.

Majaliwa amezitaka mamlaka hizo kuendela kutoa mafunzo ya uhamasishaji ya matumizi ya nyenzo mpya za usimamizi na uwekezaji pamoja na kuhakikisha jamii inashirikishwa katika mchakato wa uboreshaji wa sheria hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live