Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu: Tumeshalipa Sh524 bilioni za korosho

40575 WAZIRIPIC Waziri Mkuu: Tumeshalipa Sh524 bilioni za korosho

Fri, 8 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema jana Jumatano Februari 6, 2019 Serikali imelipa Sh100 bilioni kwa wakulima wa korosho na kufanya jumla ya malipo kwa wakulima hao kufikia Sh524.8 bilioni.

Majaliwa ametoa ufafanuzi huo leo Alhamisi Februari 7, 2019 bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wakati akijibu swali la mbunge wa Liwale (CCM), Zuberi Kuchauka.

Kuchauka amehoji kwa nini wakulima wa korosho hawajalipwa fedha zao.

Majaliwa amesema kilichochelewesha hadi sasa ni uhakiki hususan wakulima waliokuwa wana tani  zaidi ya 1,500 kwamba lengo ni kujiridhisha kama kweli ni wamiliki halali wa korosho hizo.

" Wakulima wawe na imani na Serikali. Wote watalipwa," amesema Majaliwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz