Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuchika aomba meli bandari ya Mtwara

Bandari Mtwaratt Waziri Mkuchika aomba meli bandari ya Mtwara

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu-Kazi Maalum, George Mkuchika amesema kuwa endapo bandari ya Mtwara itawezeshwa meli itakayofanya safari zake kutoka mkoani hapo kwenda katika nchi ya Comoro kutakuza mahusiano ya kibishara yaliyopo.

Kauli hio ameitoa leo Jumapili Julai 16, 2023 katika mkutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo. Mkuchika ambaye ni Mbunge wa Newala Mjini amesema kuna shauku kubwa la Watanzania kufanya biashara na nchi ya Comoro ambapo meli zikija mbili au moja zinaweza kusaidia wafanyabiashara katika azma hiyo.

“Ni vema tukapata meli kama ilivyo kwenye ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika na sisi tupate meli ili tufanye bishara na mataifa mengine, tunapokosa meli kama hizi tunakuwa hatukuzi biashara zetu kimataifa,”amesema. Ombi hilo linakuja wakati kukiwa na ugeni wa madiwani wa Kisiwa cha Anjoun kilichopo nchini Comoro wakiongozwa na Gavana wa kisiwa hicho Annis Chamsidine ambao wamekuja kuangalia fursa mbalimbali nchini ili waweze kuwekeze na kufanya biashara na nchi ya Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live