Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mku aridhishwa kasi mradi wa SGR

Reli SGRRRRRRR Waziri Mku aridhishwa kasi mradi wa SGR

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha mradi huo unajengwa kwa viwango na kukamilika kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.

Amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri katika vipande vyote na kwamba Serikali itahakikisha mradi huo haukwami na itakabiliana na viashiria vyote vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wake.

Ameyasema hayo jana, Novemba 24, 2022 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni kuu ya Dodoma katika eneo la Mkonze, jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni hiyo, Majaliwa amewataka Watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo wasimamie usalama wa mradi na wawe walinzi ili ukamilike kama ilivyokusudiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live