Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkenda: "Sitoi kibali cha kuagiza sukari"

Waziri Mkenda Waziri wa kilimo Adolf Mkenda

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia tatizo la uhaba wa Sukari nchini, Waziri wa kilimo Adolf Mkenda amesema kuwa hatatoa kibali cha uingizaji wa Sukari Nchini kwa wafanya biashara wa sukari.

Wziri Mkenda ameyasema hayo, kwenye uzinduzi wa matokeo ya sensa ya kilimo ,mifugo na uvuvi ya mwaka 2019/2020, jijini Dodoma

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mkenda amesema uingizaji wa sukari kutoka nje unawafanya wakulima kutouza miwa kwenye viwanda vilivyopo hali inayowakwamisha wafanyabiashara wa miwa, hivyo zuio la vibali litasaidia kuwainua wakulima na kuongeza uzalishaji kwenye viwanda vya sukari vya ndani.

Waziri Mkenda, amesema Suala la kuingiza sukari ni la rushwa na ufisadi na tamaa yakunufaisha wachache . "suala la kuingiza sukari nchini ni suala la rushwa la ufisadi mkubwa kwa sababu tamaa yake kubwa mno,tamaa ya kuwafaidisha wachache kuwanyima watanzania ajira kubwa mno"amesema Prof.Adolf Mkenda

Waziri amewataka wafanyabiashara waache kuwasumbua bodi ya sukari kwani kwa sasa yeye ndiye anayehusika na utoaji wa vibali na hatotoa kibali kwa mfanyabiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live