Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkenda: "CPB fanyeni biashara ya mahindi nje ya nchi"

Mahindi Waziri wa Kilimo Adolf Mkenda

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) nchini imetakiwa kufanya jitihada za ziada katika kuyaongezea thamani mazao ili kuweza kushindana na soko la nchi za nje.

Hayo yamesemwa na waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda wakati akizindua viwanda vya bodi hiyo ya mazao mchanganyiko vilivyozinduliwa katika jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema CPB inachukua majukumu ambayo yalishindwa kutekelezwa na GAPEX iliyokuwa imepewa majukumu ya kuchakata na kuuza mahindi nje ya nchi.

CPB imechukua majukumu ambayo huko nyuma kulikuwa na GAPEX (kwa ajili ya kuuza mazao nje ya nchi) na National Milling Corporation (kwa ajili ya kuchakata nafaka), lakini walishindwa kuziendesha.  

“Taasisi hizi zilikuwa kubwa National Milling Corporation ni taasisi kubwa sana ilianza kwa kufanya kazi kubwa sana hapa nchini baadaye ikawa mzigo na matokeo yake ikafa, na mali zilizobaki chache ndio hizo ambazo mnazo CPB, GAPEX pamoja na kuwa soko la mazao lipo ikawa mzigo na ikafutwa majukumu hayo mmepewa nyie CPB,” alisema.  

Alibainisha kuwa kufa kwa taasisi hizo kulitokana na kufanya maamuzi mengi kufanyika kwa misingi isiyokuwa ya kibiashara.  

"Mwelekeo wenu kwa sasa ni mzuri unatupa matumaini kwamba hamtashindwa tena kama kwenye National Milling na GAPEX, naona uwekezaji unaenda, nimeona uchakataji wa korosho, naona mna kiwanda pale Dar es Salaam cha kuchataka korosho ili isiuzwe korosho ghafi," alisema Prof. Mkenda.  

Amesema serikali itaisaidia bodi hiyo ifanye maamuzi yake kwa misingi ya kibiashara ili wasikumbane na anguko la taasisi zilizokufa.  

Chanzo: ippmedia.com