Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Makamba azindua bodi ya wakurugenzi TPDC

January Makamba TPDC Waziri Makamba azindua bodi ya wakurugenzi TPDC

Mon, 4 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati January Makamba amezindua bodi ya wakurugenzi wa shirika la petroli (TPDC) ambayo itachochea kasi ya ukuaji wa maendeleo katika shirika hilo.

Akizindua bodi hiyo jijini Arusha leo Waziri Makamba amesema kuwa ,uteuzi wa bodi hiyo una akisi dira na malengo mapya ya serikali kwa shirika hilo kuelekea katika mafuta na gesi.

Amesema kuwa,bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wake Balozi Ombeni Sefue inakidhi nafasi ya TPDC katika maendeleo ya nchi, dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa Gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.

Amesema kuwa, maendeleo ya sekta ya mafuta na Gesi nchini yapo katika dhamira ya kulisaidia Taifa kufikia kuweza kuleta mchango kwa serikali kuanzia ngazi ya mapato na miradi mikubwa ya kimkakati.

“dhamira yetu ni kuona Shirika hili linatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu bali uendeshaji wa Rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu amesema wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda inavyotakiwa na sekta hii ili Taifa liweze kunufaika na Rasilimali zake za mafuta na Gesi.

“Mikakati iliyopo kwa sasa ni ile ya serikali na haijaanza leo tutaipitia kama bodi mpya tumefanikiwa na changamoto ni zipi na zitatatuliwaje ili kazi iendelee vizuri kujenga TPDC yenye kusaidia serikali.”amesema.

Awali Mkurugenzi wa Shirika la mafuta na Gesi nchi James Matagio amesema kuwa, miradi ya mafuta na Gesi itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi.

Amesema kuwa, wana miradi mikubwa ya uchakataji wa Gesi asilia ambao unatarajiwa kujengwa kwa viwanda na utagharimu takribani shs 40 bilioni ikiwemo pia mradi wa kujenga Bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda ambao umeonyesha mafanikio tokea umeanza pia Kuna mradi wa kutafuta mafuta katika bonde la ufa ambao upo kwenye Mchakato kwa awamu ya kwanza ya uchimbaji.

Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa petroli nchini,(PURA)Injinia Charles Sangweni amesema kwamba uundwaji wa bodi ya shirika la TPDC utasaidia Sana kuleta tija na maendeleo katika mamlaka yao hususani upande wa maamuzi kwani imekaa muda mrefu bila kuwa na bodi na taasisi yoyote isipokuwa na bodi inakuwa haijakamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live