Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Kijaji atembelea gari la 'Masoud Kipanya'

Kijaju Kijaji akiwa ndani ya gari ya Masoud

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji amemtaka Mtanzania Mbunifu Masoud Kipanya kuandika barua SIDO ili waweze kuwaandikia TBS na kuweza kutoa Cheti cha Ubora wa gari ambalo amelibuni hivi karibuni.

Ameyasema hayo leo Waziri Kijaji mara baada ya ziara yake katika Shirika la Viwango Tanzania na kujionea gari ambalo amelibuni Masoud Kipanya likifanyiwa tathimini ya ubora wa viwango ili mbunifu huyo aendelee kuzalisha magari mengine yenye ubora unaotakiwa.

Amesema kuna mambo madogo yanahitaji kurekebishwa kwenye gari hilo hivyo Masoud Kipanya atakaa na wahandisi wa TBS ili waweze kuelekezana ili gari liweze kupita katika barabara zote kwani jinsi ilivyo inaweza ikapita na ikaumia kwa muda mfupi.

“Tunataka kukaa nae ili aweze kutengeneza chombo ambacho sasa kitaweza kutumika kwenye uhitaji wa soko letu lilivyo na sisi kama wizara tunasimamia kuona anafikia kwenye viwango vizuri na kwa mara ya kwanza tuseme tuna gari letu ndani ya taifa letu”. Amesema Waziri Kijaji.

Aidha Waziri Kijaji amesema wanawatambua wote wabunifu ambao wapo katika jamii na wizara imejipanga kuanza kuwafikia vijana wabunifu wakitanzania kuanzia kwenye fikra zao mpaka kufikia kuwajenga hatua kwa hatua.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Mhandisi Johanes Maganga amesema wanaendelea kutekeleza majukumu yao na mpaka sasa matokeo ya awamu ya kwanza yameshatoka na maelekezo ambayo wamepatiwa na Waziri wanaenda kuafanyia kazi kuanzia sasa.

“TBS kwa kushirikiana na Masoud Kipanya tutakaa nae tutaangalia ninamna gani ambavyo anaweza akafanya malekebisho hayo kwa muda mfupi kwamaana hatutaki achelewe alafu aanze uzalishaji wa magari mengine ambayo ameshaanza kuyatengeneza”. Amesema

Pamoja na hayo Mhandisi Maganga amesema wanategemea kuona gari la Masoud Kipanya linakuwa na ubora unaotakiwa kama magari mengeni ambayo yaagizwa kutoka nje ya nchi lakini kwa taifa yeye kuzalisha magari ni faida kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live