Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) nchini kuhakikisha anashughulikia suala la kupanda kwa bei ya mitungi ya gesi nchini ndani ya kipindi cha siku 14 kuanzia leo Agosti 10
Dkt.Kalemani ameyasema hayo Wilayani Chato Mkoani Geita wakati wa uzinduzi wa kongamano la uzinduzi wa bomba la mafuta ghafi litakalojengwa kutoka Uganda mpaka Tanzania litakalogharimu kiasi cha USD 3.2.
Dkt. Kalemani amewataka Wakurugenzi wa EWURA pamoja TPDC kuweka matangazo yao ya kazi kwa lugha ya kiswahili ili kuepukana na changamoto ya wasiojua lugha ya kiingereza.