Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga amehoji sababu za taasisi za fedha kupunguza kiasi cha mikopo inayoelekezwa kwenye sekta ya kilimo.
Amesema kwa mwaka 2018 mikopo inayokwenda kwenye sekta hiyo imefikia asilimia 5.7 kiwango ambacho kinaendelea kupungua mwaka hadi mwaka.
Hasunga amehoji hilo leo Ijumaa Agosti 31,2019 wakati wa mkutano wa wasindikaji, wasafirishaji na wamiliki wa maghala unaofanyika jijini Dar es Salaam.
“Nataka kufahamu kwa nini mikopo inayoelekezwa kwenye sekta ya kilimo inazidi kupungua, taasisi za benki mmejipangaje kuongeza hili,” amesema
Akijibu swali huko mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo (TIB) Patric Mongela amesema kuna changamoto ya taarifa kuwafikia wakulima jambo linalowafanya wachache kufahamu kuhusu fursa ya mikopo.
“Kuna haja ya elimu ya kifedha kutolewa kwa wakulima hasa wadogo, wengi hawafahamu kuhusu mikopo na ukweli ni kwamba wachache ndio wanawekeza kiasi kikubwa kwenye kilimo,” amesema
Pia Soma
- Wakili wa kina Mbowe ashindwa kufika mahakamani, kesi yaahirishwa
- Mahakama yamtaka wakili kesi ya kina Mbowe kufika mahakamani ndani ya saa moja
- UPDATE: Kinachoendelea Afrika Kusini kukamatwa kwa ndege ya ATCL
Amesema ipo haja ya Serikali wakati wa mapitio ya sera ya kilimo kuwahusisha wadau wa taasisi za fedha ili kutoa mawazo yao.
“Mheshimiwa waziri hakuna haja ya kumung’unya maneno mabenki hayatoi mikopo kwenye kilimo kwa sababu ya risks zilizopo. Wakulima wanategemea mvua sasa isiponyesha ni balaa,” amesema