Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Hasunga aagiza mrajisi kukamatwa, kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

90157 HASUNGA+PIC Waziri Hasunga aagiza mrajisi kukamatwa, kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sumbawanga. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Japhet Hasunga ameagiza kukamatwa kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Rukwa, Anyosisye Mbetwa kwa tuhuma ya kushirikiana mmoja wa mawakala wa pembejeo za kilimo kutapeli vyama vya ushirika zaidi ya Sh277 milioni.

Ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Desemba 27, 2019 wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika (Amcos) mkoa wa Rukwa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo Sumbawanga Mjini.

Pamoja na mrajisi huyo, pia ameagiza kukamatwa kwa wakala Elias Ndomba mkurugenzi wa kampuni ya Eli Agrovet Co ambao waliahidi kufikishia mbolea wakulima hao kupitia vyama vyao vya ushirika.

Waziri Hasunga amesema mrajisi huyo ambaye ni ofisa ushirika wa mkoa huo kwa makusudi amekiuka sheria, kanuni na taratibu za vyama vya ushirika hivyo amemshusha cheo hicho na sio ofisa ushirika tena.

Amesema ofisa ushirika huyo amepoteza sifa ya kuendelea kuwapo katika nafasi hiyo kwa kula badala ya kuwasaidia wanaushirika yeye anashiriki kuwahujumu.

"Naagiza hawa wote wakamatwe mara moja kwa kuwa wamewatapeli sana ushirika kwa kuchukua fedha zao pasipo kuleta mbolea, labda wakileta mbolea hapa ndiyo waachiwe tofauti na hivyo wafunguliwe mashtaka ya kuhujumu uchumi," amesema Waziri Hasunga.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Ufipa, Anastela Malaji akizungumza kwa niaba ya Amcos 49 kiliingia mkataba na kampuni ya Eli Agrovet ya kusambaziwa mbolea kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali amedai mrajisi aliwataka watoe fedha asilimia 30 ya mbolea waliokuwa wakihitaji.

Amesema makubaliano ilikuwa kampuni hiyo iongeze fedha asilimia 70 kisha kununua mbolea na kuwafikishia wakulima lakini baadaye iligundulika haikuwa na mtaji huo hivyo kuchukua fedha hizo za kwao kununua mbolea kiduchu aina ya Dap na kuwapelekea kinyume na makubaliano yao.

Imeelezwa makubaliano baina ya chama hicho na kampuni hiyo ilikuwa inunue mbolea ya Dap, Urea na Can na kusambaza kwa wakulima ili waweze kuzalisha mazao yao kwa tija.

Chanzo: mwananchi.co.tz