Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Biteko kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii UN

1647513085922 1080x640 Dakta Biteko akiwa na Rais wa Baraza la Uchumi

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko amekutana na Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC), Collen Kelapile katika kikao kilicholenga kupata maelezo kabla ya kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika tarehe 18 Machi, 2022, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Tanzania inashiriki katika kikao hicho ikiwa ni Mwenyekiti wa Nchi Wazalishaji wa Madini ya Almasi Afrika ADPA.

Aidha, kikao hicho kinalenga kujadili namna bora za kutumia rasilimali katika nchi husika kuibua maendeleo jumuishi kwenye jamii ambazo maliasili hizo zinapatikana ili zisaidie kuleta amani na hatimaye kufikiwa maendeleo endelevu.

Kikao hicho kitafanyika chini ya mada isemayo ‘Maliasili Jamii yenye Amani na Maendeleo Endelevu: Mafunzo kutoka kwenye Mchakato wa Kimberley’

Wengine wanaoshiriki kikao hicho katika picha ni pamoja na Waziri wa Madini wa Zimbabwe Wiston Chitando ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ADPA, Mratibu wa Kimberly Afrika Jacob Thamage na Mwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mataifa, Balozi Prof.Kennedy Gastorn.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live