Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri: Bila fedha mkononi hakuna kufanya uthamini wa ardhi

Ardhipiic Data Waziri: Bila fedha mkononi hakuna kufanya uthamini wa ardhi

Sun, 5 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hayo yamesemwa jana Jumamosi Juni 4, 2022 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Waziri Mabula amesema wanafanya hivyo kwa  kuwa  hilo limekuwa moja ya sababu za kuongezeka  kwa kesi za migogoro  ardhi licha ya sheria kueleza muda  wa kuwalipa watu tangu uthamini ulipofanyika kuwa ni miaka miwili.

"Hili la uthamini nalo ni eneo jingine lenye kuchangia migogoro ya ardhi, niwaeleze tu leo ambao mnahitaji ardhi ya wananchi kwa ajili ya kufanyia shughuli zozote mhakikishe mnakuwa na hela mkononi ndio tuingie kwenye uthamini."

"Sheria ya ardhi ya mwaka 2017 imeeleza wazi kwamba anayefanyiwa uthamini anatakiwa kulipwa ndani ya miaka miwili tangu amefanyiwa uthamani,lakini badhi ya watu hawafanyi hivyo," amesema Waziri Mabula.

Amebainisha kuwa wanaotakiwa kulipwa ndani ya miaka miwili ni wale waliochukuliwa maeneo yao kuanzia mwaka wa 2017 ambapo sheria hiyo ilianza kutumika rasmi baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Advertisement "Awali kabla ya kufanyiwa marekebisho sheria ya ardhi ilitaka mthaminiwa kulipwa ndani ya miaka kumi lakini baadaye ilifanyiwa marekebisho na kuanza kutumika rasmi Januari 2017 ," amefafanua waziri huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live