Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Bashungwa amteua bosi wa Brela

92407 Pic+brella Waziri Bashungwa amteua bosi wa Brela

Mon, 20 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashaara nchini Tanzania, Innocent Bashungwa amemteua Godfrey Nyaisa kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).

Taarifa iliyotolewa jana Jumapili Januari 19, 2020 na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ludovick Nduhiye imesema Nyaisa anachukua nafasi ya Loy Mhando ambaye alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Nyaisa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia wajibu alionao kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1977 Sura 245 Kifungu 9(1) kama ilivyorekebisha mwaka 2009” imesema taarifa hiyo.

 

Taarifa hiyo imesema uteuzi huo wa Nyaisa umeanza rasmi Jumapili Januari 19, 2019.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz