Tabora.Waziri wa Biashara na Viwanda,Innocent Bashungwa,ameonesha kukerwa na kutofanya kazi kikamilifu, kiwanda cha Nyuzi Tabora na hivyo kutofikia lengo la Serikali la kutaka kuwa na uzalishaji mkubwa wa Nyuzi na kuongeza ajira.
Akizungumza baada ya kukagua shughuli zinazofanyika kiwandani hapo,Waziri huyo, amesema hajaridhika na utendaji kazi wa kiwanda hicho na malengo ya Serikali hayajafikiwa.
"Ubinafsishaji ulikuwa na nia njema na bahati mbaya hapa nimekuta ubabaishaji" Amesema
Amesema inaelekea waliochukua kiwanda hicho,hawqkuwa wamejiandaa na kisema wazi kuwa hajaridhika na utendaji kazi wa kiwanda hicho.
Amesema Serikali itaangalia namna kitakavyoweza kuzalisha kwa tija na kukitaka kiwe tayari kubadilika kwa lengo la kutimiza azma ya kubinafsishwa kwake.
Katibu tawala wa Mkoa wa Tabora, Msalika Makungu,amesema wamiliki hata taarifa zake hazipo wazi na hivyo kuwa vigumu kuona namna ya kisaidia.
Pia Soma
- Harmonize kuiwakilisha Afrika Mashariki tuzo za MTV Europe Music Awards 2019
- Wamiliki kiwanda cha Nyuzi walalamikia ukosefu wa masoko
- Pundamilia wa ajabu ahamia Tanzania akitokea Kenya