Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazalishaji mafuta ya kula wapongeza uondoaji VAT

Mafuta Ya Kula Wazalishaji mafuta ya kula wapongeza uondoaji VAT

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wasindikaji Mafuta ya Kula ya Alizeti Tanzania (TASUPA) kimesema hatua ya serikali kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwa mafuta ya kula kwa kutumia mazao yanayozalishwa na wakulima nchini itahamasisha uwekezaji wa viwanda vya kuongeza mazao ya kilimo.

Pia, kimepongeza hatua ya serikali kutoa mapendekezo ya kuanza kutoza ushuru wa forodha kwa mafuta ya kula yanayoagizwa kutoka nje.

Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Ringo Iringo alibainisha hayo jana jijini hapa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyopendezwa na Waziri wa Fedha, Dk. Mwingulu Nchemba wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Iringo alisema serikali kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwa mafuta ya kula kwa kutumia mazao yanayozalishwa na wakulima nchini itahamasisha uwekezaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo nchini.

Vile vile, alipongeza serikali kwa kupendekeza katika bajeti yake iliyowasilishwa kwa mwaka fedha 2024/25 kuanza kutoza ushuru wa forodha kwa mafuta ya kula yanayoingizwa toka nje kwa asilimia 25 au 35 au Dola za Marekani 250 kwa tani kwa mafuta ghafi au Dola za Marekani 500 kwa tani kwa yaliyosafishwa.

Kadhalika, alisema sekta ndogo ya mafuta imekuwa kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutoka na juhudi na afua mahususi zinazofanywa na serikali na wadau wa maendeleo.

Alisema viwanda hivyo vinauwezo wa kukamua kwa asilimia 100 jumla ya tani za ujazo 5,000 kwa siku, hivyo kuhitaji tani za ujazo 1,800,000 kwa mwaka za alizeti.

Alisema TASUPA, inauthibitishia umma kuwa ifikapo mwaka 2027 changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini itakuwa imeisha na kuanza kuuza nchi za nje ka kama Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Comoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live