Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazalishaji binafsi wa umeme Tanzania waonywa

86449 Pic+umeme Wazalishaji binafsi wa umeme Tanzania waonywa

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Nishati nchini Tanzania,  Dk Medard Kalemani amewataka wazalishaji binafsi wa umeme wanaotoza gharama kubwa ya nishati hiyo tofauti na iliyopangwa na Serikali kuacha kwa kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Dk Kalemani ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 29, 2019 katika kikao na makandarasi wa miradi ya nishati vijijini.

Amesema amekwenda Ukerewe na kushuhudia mzalishaji wa umeme akiwatoza wateja Sh3,500 kwa uniti bei ambayo ni tofauti na iliyopangwa na Serikali.

Dk Kalemani amesema bei ya kuunganisha umeme na bei ya nishati hiyo lazima ifanane nchi nzima bila kujali mzalishaji ama jiografia ya eneo husika.

"Mnapewa ruzuku na Rea (Wakala wa Umeme Vijijini) kwa nini mtoze bei kubwa ya umeme. Wazalishaji wakome mara moja," amesema Dk Kalemani.

Chanzo: mwananchi.co.tz