Menu ›
Biashara
Thu, 10 Aug 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amewaagiza wakurungezi watendaji wa Halmashauri kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wazalishaji wa chumvi isiyo na madini joto ya kutosha mkoani humo.
Pia amewataka wakurungezi watendaji hao kusimamia na kuhakikisha kuwa chumvi zinazozalishwa na kusambazwa ndani ya mkoa zinafanyiwa uchunguzi wa kimaabara, ili kubaini uwepo wa madini joto kulingana na miongozo ya serikali.
Abbas ametoa maagizo hayo leo Agosti 10 wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live